Watoto wanatajwa kuwa ndio hazina ya taifa la kesho. Watoto ndio jamii inayotegemewa kwa kizazi cha kesho. Hata hivyo pasipokuwa na usimamizi imara pamoja na mikakati iliyo thabiti ya kuwalinda watoto, ni wazi tunalibomoa taifa la kesho. Hivyo basi wale wanaowania kupewa dhamana kwenye nyadhifa mbalimbali ni wazi watakuwa wanasimamia misingi iliyo bora ya kuwalinda watoto.

Watoto hawa wanapaswa kulindwa katika Nyanja mbalimbali kuanzia katika hatua yao ya awali yaani kabla na baada ya kuzaliwa. Kwa lugha nyepesi tunapaswa kuwa linda watoto na wanawake pia.

 

walinde watoto

SOMA ZAIDI:

 

Katika miradi ambayo imekuwa ikiendeshwa na True Vision production chini ya taasisi ya walindewatoto.org. Mambo kadha yanatajwa kuwa ndio msingizi wa kuwawezesha watoto katika kufikia malengo. Mambo hayo ni kama,

  1. Kuwekeza kwenye lishe bora

Inatajwa kuwa katika kila watoto 10 wa kitanzania basi watoto 3 hawafikii kiwango cha ukuaji kimwili na kiakili kwa sababu ya utapiamlo. Hivyo basi jamii inapaswa kuwekeza kwenye upatikanaji wa lishe bora kwa watoto na akina mama.

  1. Kuwekeza kwenye huduma bora za maji na usafi wa maingira hasa vyoo mashuleni.  

Upatikanaji wa maji na vyoo vilivyo bora mashuleni ni wajibu na serainayopaswa kusimamiwa ili kuwawezesha watoto kupata elimu kwenye mazingira yaliyo salama.

  1. Kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wote

Suala la elimu bora pia linapaswa kutiliwa mkazo kwa watoto, kwakuwa watoto ndio taifa la kesho. Misingi iliyo bora na urithi thabiti kwa mtoto ni elimu, hiyvo basi mikakati thabiti lazima iweke katika kuwalinda watoto ili waweze kupata elimu ilyo bora.

  1. Kuwekeza katika kupunguza mimba za utotoni

Mimba za utotoni limekuwa janga kubwa sana kwa watoto. Jamii pamoja na viongozi husika wanapaswa kuwekea misingi iliyo bora katika kuwalinda watoto na janga hili la mimba za utotoni.

  1. Kuwalinda watoto wachanga na wasichana dhidi ya VVU

Tunapaswa pia kuwalinda watoto wachanga na wasichana dhidi ya maambukizi ya “Virusi Vya UKIMWI” ili kuwafanya watoto wawe salama zaidi, jamii yote kijumla pamoja na viongozi wenye dhamana wanapaswa kutengeneza sera na mikakati ya kuwakomboa watoto kwenye janga hili, ili kuokoa watoto ambao ndio taifa la kesho.

Ni wazi kiujumla kila mmoja anapaswa kusimamia misingi na sera zilizowekwa ili kuwatengenezea watoto mazingira yaliyo salama. Watoto wanapaswa kulindwa daima.