Maadhimisho ya siku ya Vijana kimataifa nchini Tanzania yanatarajiwa kufanyika Agosti 15 hadi 16 mjini Dodoma, huku maudhui ya siku hiyo yakienda sambamba na ujumbe unaosema, Kuelekea 2030, Tanzania ya viwanda: Boresha elimu kwa vijana, kwa maendeleo ya Taifa.

Ni wazi kuwa vijana wanatajwa kuwa ndio chachu ya maendeleo ya nchi hasa katika kuelekea uchumi wa kati. Vijana wanatajwa ndio wabeba dhana ya maono ya 2030 kuelekea uchumi wa Viwanda.

True Vision Production ikishirikiana na ANSAF wamekuandalia kipindi maalumu cha Vijana na Kilimo biashara.

Kutana na kijana Mjasiriamali wa kilimo cha Mboga mboga, Machel Tarimo ambaye awali alikuwa anafanya kazi kama Mhasibu kwenye kampuni fulani kabla ya kuamua kuachana nayo na kufungua kampuni ya Home Veg, Tanzania akishirikiana na wenzake kadhaa.

SOMA ZAIDI:

Akiwa kama Mhasibu bwana Machel Tarimo alifanya kazi kwa miaka 8 na kabla ya kuanzisha kampuni ya Home Veg Tanzania ambayo uchukua mazao ya mboga mboga kwa wakulima wadogo na kupeleka kwenye masoko ya nje ya nchi.

Home Veg. Tanzania haifanyi shughuli ya kilimo bali inawawezesha wakulima wadogo waweze kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa kwenye soko la Ulaya. Home Veg. Tanzania uyachukua mazao na kuyachanganua kabla ya kuyafungasha kwa ustadi (Grading and Packing) kwa ajili ya kuyasafirisha kwenda nje ya nchi.

kilimo biashara

Wakulima wa mboga mboga sasa nao wana uhakika wa soko lao ukilinganisha hapo awali. Hii ni kutokana na uwepo wa Home Veg. Tanzania mabo huyachukua mazao yao na kuyaongeza thamani kabla ya kuyasafirisha nje ya nchi.

Vijana na Kilimo Biashara ni mradi maalumu unaofanywa na kampuni ya True Vision Production wakishirikiana na ASAF ambapo uangazia vijana katika shughuli nzima ya kilimo na biashara.

Kilimo biashara

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na True Vision Production tafadhali wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.