Suala la afya ya uzazi ni jambo la kuzingatiwa na kila mmoja wetu katika kuepusha vifo vinavyojitokeza kutokana na uzazi. Takwimu zinaonysha akina mama wengi wajawazito hupoteza maisha wakati wa kujifungua. Familia zaidi ya 9,000 kila mwaka zinapoteza akina mama.

Ripoti mpya ya jamii na afya (DHS) ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya mwaka 2015/2016 inaonyesha kuna vifo 556 vya uzazi katika kila vizazi hai 100,000. Kiwango hiki ni kikubwa ukilinganisha na ripoti ya mwaka 2012 ambapo wanawake 432 walikufa kwa uzazi

Ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya millennia kuhusu afya ifikapo mwaka 2030 ya kuwa na raia wenye afya bora, ni wazi sasa kila mmoja wetu ana mchango wa kuhamasisha akina mama kuhudhuria kliniki katika kipindi chote cha ujauzito na cha kujifungua.

SOMA ZAIDI

Jamii inapaswa kuhimiza akina mama kujifungulia hospitali, ili kuepuka vifo vya akina mama na watoto vinavyotokana na wao kuamua kujifungulia nyumbani.

Lakini pia inapaswa kuwaelimisha kina mama umuhimu wa kuhudhuria kliniki mapema mara tu wanapojigundua wana ujauzito, ili kujiepusha na athari mbalimbali zinazoweza kutokezea wakati wa kujifungua.

  • Ili kulipa nguvu suala hill, NHIF wamezindua mradi maalumu ujulikanao kama ‘ NHIF na Kfw’ unaomuwezesha mama mjazito kujifungulia hospitali pamoja na kupata huduma stahiki za matibabu pamoja na familia yake.

Mpango wa NHIF na Kfw  

  1. Mama mjamzito atapewa kadi iliyolipiwa na NHIF mpaka atakapojifungua. Na ataendelea kutumia kadi miezi 3 baada ya kujifungua yeye pamoja na mtoto wake.
  2. Familia itapewa kadi ya CHF ya matibabu bure kwa mwaka mzima.

Vifo vya akina mama wajazito na watoto vinaepukika, jamii haina budi kuchukua hatua ili kunusuru akina mama na watoto.

Kwa kushirikiana na Mfuko wa Afya ya Jamii pamoja na Kfw Entwicklungsbank. True Vision Production imeandaa mchezo wa kuigiza wenye lengo la kuelimisha jamii kuhusiana na mpango wa Kfw.