True Vision Production (TVP) kama ilivyo kawaida yake, imekuwa ikishiriki katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Ushiriki wake kwa namna moja ama nyingine unalenga kutoa taarifa zenye uelewa juu ya mradi husika hasa katika upande wa uandaaji wa vipindi na Makala mbalimbali.
Moja ya mradi ambao TVP imepata nafasi ya kushiriki ni pamoja na ule wa Matokeo Makubwa sasa “Big Result Now” (BRN). Mpango huu ulianzishwa Julai Mosi, 2013 chini ya ofisi ya Rais. Ili kuweza kufikia malengo ya dira ya Taifa yamwaka 2025 kwa kuweka vipaumbele katika sekta muhimu katika uchumi wa Taifa. Huku malengo yakiwa ni kuleta mabadiliko, motisha na nidhamu mpya katika kutekeleza miradi ya kipaumbele.
Moja ya sekta muhimu ya kipaumbele katika mpango wa BRN ni sekta ya nishati na gesi. Sekta ambayo imepewa kipaumbele ili kuweza kusaidia Taifa kuondokana na adha ya nishati ya umeme. Mpango huu unajumuisha uwekaji wa bomba la gesi asilia la mtwara. Mradi ambao unatekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Taifa kupitia shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC).
True Vision Production (TVP) ilipata nafasi ya kusafiri hadi mkoani Mtwara ili kuweza kuufikia mradi huu mkubwa. Moja ya malengo ya safari hii ilikuwa ni kuweza kuandaa vipindi na Makala mbalimbali zinazoonyesha uaandaji na umuhimu wa uwepo wa mradi huu kwa Taifa.
Kipindi maalumu cha Utekelezaji wa Mradi wa Nishati ya gesi asilia.