Ni wazi kuna kampuni nyingi za uzalishaji wa vipindi mbalimbali ya radio na televisheni. Lakini linapokuja suala la umahiri wa kazi ni wazi kampuni ya True vision Production (TVP) imepiga hatua kubwa mno. Umahiri katika utendaji kazi zake ni wazi ndio chachu ya mafanikio chanya.
Ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika uzalishaji wa filamu, matamasha, matangazo ya biashara ya TV / Radio, Magazeti, Video na makala za Tv na redio pamoja na uandaaji wa kampeni mbalimbali za Uelewa na mabadiliko ya kitabia (Awareness and behaviour change Campaign.)
True Vision imekuwa moja ya kampuni ya Video Production inayoongoza kwa kipindi kirefu. Hii ni kutokana na sifa yake kubwa ya kutoa huduma stahiki na iliyobora kwa wateja wake (Serikali, Sekta binafsi, NGO pamoja na mashirika ya kimataifa.
Ni kampuni inayoundwa na timu yenye ujuzi na uzoefu katika taaluma. Timu yenye kuwa na ubunifu wa kazi mbalimbali zenye kuweza kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira lengwa.
Zipo kazi mbali mbali ambazo si ngeni katika macho ya watu wengi. Kazi ambazo zimefanywa kwa ajili ya kuelimisha jamii pamoja na kuamsha jamii.
Licha ya kufanya kazi kwa bidiii, TVP pia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuzalisha rasilimali watu ambao wanatumika sasa kwenye baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari.
Hivi ni nani ambaye hajaona kazi zinazofanywa na TVP?. Hebu angalia kampeni hii hapa chini ya Motisha kwa waalimu, iliyo chini ya Haki elimu.
Na je, umeshawahi kuona vipindi mbalimbali ya Hifadhi za Taifa na vivutio vyake?
Naam ni wazi umepata kuona kazi hizo. Kwa ufupi TVP inafanya kazi katika mazingira mbalimbali hasa maeneo ya vijijini ambayo wengine imekuwa vigumu kuyafikia.