Dar es Salaam. Watoa huduma za afya nchini wameaswa kuzingatia maadili ya kazi ikiwemo kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa hasa kwa wamama wajawazito ili kuepusha vifo vya akina mama wajawazito visivyo tarajiwa.
Akichangia mada kwenye semina maalum ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto, inayojulikana kama “Jiongeze Tuwavushe Salama” Mwakilishi wa BAKWATA, sheikh wa msikiti wa Manyema, jijini Dar es salaam Sheikh Hamid Masoud Jongo amesema kuna malalamiko kuwa baadhi ya watoa huduma wanakuwa na lugha mbaya kwa wagonjwa
“Kuna maoni kwamba baadhi ya watoa huduma wanakua na lugha mbaya kwa wagonjwa. Kuna umuhimu wa kushughulikia hili”-Alisema Sheikh Jongo
SOMA ZAIDI
- Mchungaji: Lishe bora muhimu kuokoa vifo vya mama wajawazito na watoto
- NKOMA: UZAZI USIWE TIKETI YA KIFO KWA MAMA NA MTOTO
- Wahariri waombwa kutumia vyombo vyao kutoa elimu ya kuzuia vifo vya mama wajawazito na watoto
Kwa upande Mwingine mwakilishi huyo wa BAKWATA hakusita kulikemea suala zima la rushwa katika huduma za afya. Ambapo amesema kuwa suala la rushwa linapaswa kushughulikiwa kwa umakini Zaidi. Kwani limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa vifo vya akina mama wajawazitom nchini.
“Pia swala la rushwa katika huduma za afya lishughulikiwe. Rushwa inachangia kusababisha vifo vya akina mama wajawazito. Baadhi ya wauguzi wanatoa huduma stahiki kwa wagonjwa wanaotoa rushwa tu. Hii sio sawa.”-Aliongeza
Kwa mujibu wa takwimu kutoka idara ya mawasiliano ya UNICEF. Tanzania ni nchi ya 9 kati ya nchi 10 Duniani zinazoongoza kwa vifo vya mama wajawazito na watoto. Huku Zaidi ya 50% ya watoto walio chini ya miaka 5 wanakufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa huku 40% kati yao ni watoto wachanga.
Kampuni ya True Vision Production (TVP) kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliandaa semina maalumu kwa ajili ya kuzindua kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto iliyofanyika katika Hotel ya Regency, Jijini Dar es Salaam ikihusisha makundi matatu, wahariri, viongozi wa dini na waandishi wa Habari
#JiongezeTuwavusheSalama
#JiongezeTuwavusheSalama
UNICEF TANZANIA