Lishe bora ni muhimu sana kwa watoto. Kufanya maamuzi maalum juu ya lishe ya watoto ni kitu muhimu sana. Msingi wa afya bora huchangiwa na lishe bora. Suala la lishe bora kwa mtoto ni muhimu na linapaswa kuzingatiwa. Kupitia mradi wa Pamoja tuwalee utafahamu jinsi gani akina mama mkoani Singida walivyojikwamua na suala la lishe bora kwa watoto.
Akina mama wa Tonge mkoani Singida wamekuwa wakipata shida sana kuhusu suala la lishe kwa watoto. Ukosefu wa elimu pamoja na hali duni ya maisha imekuwa kikwazo kikubwa katika kutafuta lishe bora kwa watoto.
Kupitia mradi wa“pamoja tuwalee” ulio chini ya USAID, SCID pamoja na Africare akina mama wa Tonge mkoani Singida wamepata suluhisho la ukosefu wa lishe bora kwa watoto.
Sasa akina mama wa Tonge wameunda vikundi vya pamoja vya kujitolea vinavyosaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa ajili ya kuwakomboa akina mama ili kuweza kupata lishe iliyo bora kwa watoto wao. Vikundi hivi vinawanufaisha akina mama kwa kuwapatia fedha inayowawezesha kujipatia lishe bora kwa watoto wao.
True Vision production ilitembelea maeneo ya kijiji cha Tonge mkoani Singida kwa ajili ya kuandaa vipindi maalumu. Vipindi vilivyo chini ya mradi wa “pamoja tuwalee” Vipindi hivi vinaelezea juhudu za mashirika mbalimbali katika kutatua tatizo la ukosefu wa lishe bora kwa watoto katika maeneo mbalimbali nchini.