Upatikanaji wa lishe bora unatajwa kuwa na nafasi kubwa katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga, kama ilivyoelekezwa na Mchungaji Christosiler Kalata, alipokuwa akichangia mada kwenye warsha maalum ya viongozi wa dini inayolenga kujadili nafasi za viongozi hao katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto iliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Akizungumza moja kwa moja kwenye semina hiyo, Mchungaji Christosiler Kalata wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Mbezi Beach amesema suala la lishe bora ni suala mtambuka ambalo kila jamii inapaswa kulizingatia ili kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga.
“Lishe bora ina nafasi kubwa katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga. Tuelimishe jamii juu ya umuhimu wa kula chakula bora, kwa wakati na kwa kiwango kinachohitajika.”-Alisema Mchungaji Christosiler Kalata
SOMA ZAIDI
- Sheikh: Watoa huduma za afya waache kuwa na lugha chafu kwa wagonjwa
- NKOMA: UZAZI USIWE TIKETI YA KIFO KWA MAMA NA MTOTO
- TRUE VISION, WIZARA YA AFYA NA UNICEF WAANDAA SEMINA KWA WADAU WA AFYA WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI NA VIONGOZI WA DINI
Lakini pia Mchungaji Kalata alitolea ufafanuzi kuhusiana na suala la utandawazi ambalo yeye binafsi alilelezea kuwa ndio chanzo kikubwa cha uwepo wa mimba za utotoni ambapo kwa sasa suala la tendo la ndoa linafanyika kama biashara.
“Mimba za utotoni zinachangiwa kwa kiwango kikubwa na maswala ya utandawazi. Zamani tendo la ndoa lilikua la kificho, sahivi linatumika kibiashara. Tutoe elimu kwamba pamoja na mambo ya kisasa kuna mila na desturi nzuri za kuiga.” Mch. Kalata aliongeza; “
Takwimu kutoka idara ya mawasiliano ya UNICEF. Tanzania ni nchi ya 9 kati ya nchi 10 Duniani zinazoongoza kwa vifo vya mama wajawazito na watoto. Huku Zaidi ya 50% ya watoto walio chini ya miaka 5 wanakufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa. Huku 40% kati yao ni watoto wachanga.
Kampuni ya True Vision Production (TVP) kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliandaa semina maalumu kwa Viongozi wa Dini inayolenga kujadili nafasi za viongozi hao katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto iliyofanyika Jijini Dar es salaam.
#JiongezeTuwavusheSalama
#JiongezeTuwavusheSalama
UNICEF TANZANIA