Sanaa na ufundi ndio mtindo wa maisha tunaoishi kila siku kama binadamu. Ndio njia pekee ambapo msanii anaweza kuonyesha ubunifu wake. Nchini Tanzania wasanii wa kazi za Sanaa hasa za ufundi wametapakaa karibia nchi nzima.

Licha ya uwepo wa wasanii wengi wa kazi za Sanaa za ufundi kila kona, bado kwa kipindi cha miaka mingi tasnia hii imekuwa ikikosa thamani na hata kudharaurika kwa watu wengi. Wasanii pia wamekuwa wakifanya kazi hii tu, kwakuwa wanavipaji na ubunifu.

Kutokana na kukosa thamani kwa tasnia hii kwa muda mrefu, DataVision International wakishirikiana na Tanzania Federation of Craft and Arts (TAFCA)  pamoja na True Vision Production imeamua kuja na mradi maalumu wa utambuzi wa wasanii wa Sanaa za ufundi, TACIP (Tanzania Arts and Craft Identification project) . Ili kuweza kuwapa thamani yao kwa kuwaunganisha na soko/mteja moja kwa moja. Lengo kuu la mradi huu ni kuondoa ombwe lililopo kati ya msanii na mteja pamoja na kumleta msanii karibu na soko.

Mradi wa TACIP

SOMA ZAIDI:

Majukumu ya Mradi wa TACIP 

DataVision International akishirikiana na TAFCA watakuwa na majukumu ya

  1. Kuwatambua wasanii wa sanaa za ufundi na kuwasajili
  2. Kujenga daraja kati ya msanii na mteja ili kusaidia kwenye mauzo (Marketing)
  3. Kuendesha shughuli za kuajiri wanachama
  4. Kujenga mfumo wa taarifa za wanachama (Buliding membership database)
  5. Kuanzisha system ya kieletroniki ya kibiashara (e-Commerce Portal)
  6. Kusaidia kifedha, mafunzo na vitendea kazi

Mradin wa TACIP

Faida za Mradi wa TACIP kwa Wasanii wa Sanaa za Ufundi

Kupitia mradi huu msanii wa Sanaa za ufundia anaweza kunufaika katika mambo yafuatayo:

  1. Msanii atakuwa anafanya shuguli zake kisheria na atatambulika (Legality and Identity)
  2. Msanii ataungwanishwa na soko moja kwa moja kupitia mfumo wa Portal (Markets and marketing opportunities)
  3. Kujengewa uwezo
  4. Usaidizi kifedha na dhana za kuendeshea shughuli zao.

Kupitia mradi huu wa TACIP, ni wazi kama wasanii watauunga mkono basi wataenda kubadilisha maisha yao kupitia Sanaa za ufundi. True Vision Production kwa kushirikiana na DataVision Internationa pamoja na TAFCA imemulika kwa kina shughuli nzima za wasanii wa Sanaa za ufunundi na kuaandaa makal fupi za mchakato wa mradi huu ambao dhana yake inabebwa na ujumbe usemao JITAMBUE. TAMBULIKA. INALIPA

Wasiliana na True vision Production kwa kubonyeza HAPA.